S.L.P. 580, Mbozi, Songwe, Tanzania

Africana's Siblings Club

ASC · AFRISIC

“Dunia ni Mzazi, Ulimwengu ni Baba — Sisi Sote ni Ndugu Mmoja”

Africana's Siblings Club ni klabu ya kipekee iliyoanzishwa chini ya Developmental of the Integrated Africana's (DiA's). Ni klabu ya kimataifa, iliyo wazi kwa kila mtu, inayolenga kurudisha undugu wa kibinadamu uliopotea na kueneza ukarimu wa mataifa yote.

Makao: Dar es Salaam, Tanzania

Vijana wakiwa pamoja (picha ya mfano)

Falsafa yetu

Familia moja ya mabara

Falsafa yetu kuu ni kwamba Bara la Afrika ni Mama wa mabara yote duniani, na mabara mengine ni ndugu zake. Kwa Mzazi wao Dunia na Baba yao Ulimwengu, sisi sote binadamu ni ndugu wa damu moja.

Afrika — Mama wa mabara

Mzazi: Dunia · Baba: Ulimwengu

Ndugu zake

  • Ulaya
  • Asia
  • Amerika Kaskazini na Kusini (mapacha)
  • Australia

Mwanzilishi

Club hii ilianzishwa na Jessey Kimei, mwanzilishi wa DiA's, akiwa na lengo la kurudisha undugu wa kibinadamu uliopotea na kueneza ukarimu wa mataifa yote.

Wanachama

Tunapokea wanachama kutoka nchi mbalimbali

Hii ni klabu ya kimataifa na ya wazi kwa kila mtu. Tunapokea wanachama kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni kote bila kujali tofauti zao.

Mabara

  • Afrika
  • Ulaya
  • Asia
  • Amerika Kaskazini
  • Amerika Kusini
  • Australia

Nchi

  • Tanzania
  • Kenya
  • Nigeria
  • Afrika Kusini
  • Ujerumani
  • Ufaransa
  • Marekani
  • Brazil
  • China
  • India
  • Australia
  • na kwingineko

Rangi, kabila, dini, lugha, umri

Kila mtu anayejiona ni ndugu wa familia ya dunia anakaribishwa.

Tunaamini kuwa utofauti wetu ndio nguvu yetu.

Mwanachama wa ASC anaweza kuwa

  • Mwanafunzi
  • Mwalimu
  • Mfanyakazi
  • Msanii
  • Mjasiriamali

…mradi tu ana moyo wa undugu.

Jinsi inavyofanya kazi

Programu ya Swahili Africa

Club inafanya kazi kupitia programu kuu iitwayo Swahili Africa, yenye nguzo nne:

  1. 01

    Swahili Africa — Mijadala

    Tunaendeleza mijadala na mawasiliano kwa lugha ya Kiswahili kama lugha ya pamoja ya Waafrika wote.

  2. 02

    Ovi Program — Kujifunza

    Programu maalum kwa watu wote wanaotaka kujua na kujifunza Kiswahili, hata kama hawakijui kabisa.

  3. 03

    Kukuza Vipaji

    Tunakuza vipaji vya mawasiliano, ujenzi wa hoja, uongozi na utamaduni.

  4. 04

    Usajili wa Mbali

    Lengo la kufanya Kiswahili kisajiliwe na kutambulika mbali kimataifa kama lugha ya undugu.

Njia za utekelezaji

  • Kuunda Club za kuzungumza Kiswahili mashuleni na mitaani, kupitia outreach
  • Kubadilishana maarifa na tamaduni
  • Kuandaa matukio ya kitamaduni mtandaoni na ana kwa ana

Wito wetu kwa ulimwengu

Club hii hueneza ukarimu wa mataifa yote. Tunawaita watu wote duniani: jioneni kama ndugu mmoja.

Dunia ni moja, damu ni moja, kesho ni moja. Ukijiunga na ASC, unajiunga na familia, si tu club.Karibu uwe ndugu yetu. Karibu nyumbani.

Karibu uwe ndugu yetu

Popote ulipo duniani, unaweza kujiunga na ASC: kujifunza au kufundisha Kiswahili, kushiriki mijadala, na kubadilishana tamaduni.